Upatikanaji wa Haki ya Kujitawala ya Watu wa Kiasili: Mwongozo kuhusu Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi
Resource Key: UJESZH6W
Document Type: Report
Creator:
Creators Name:
Place: Massachusetts
Institution: Cultural Survival and First Peoples Worldwide
Date: September 2023
Language: swahili
Mwongozo huu umeandikwa ili kusaidia Watu wa Asili wanaotetea ardhi, maeneo na rasilimali zao. Unalenga kutoa mwongozo ulio wa kina kwa viongozi na jamii za watu wa asili kuhusu namna ya kutekeleza Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi. Unajumuisha mapendekezo ya kitaalamu na ya kimkakati kuhusu namna bora ya kuuendana na mifumo ya kimataifa ya mamlaka na fedha ili Watu wa Asili waweze kupata mafanikio wanapokabiliana na mifumo hiyo. Mwongozo huu umewekwa kwa mpangilio ufuatao: • Sehemu ya 1 inafananua maana ya Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi na kueleza namna watu wa asili wanavyopambana kwa mafanikio kuandika itifaki za haki hizo kwa kutoa mwelekeo wa majadiliano kuhusu Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi. • Sehemu ya 2 inaeleza hatua za ndani ambazo jamii za asili zinaweza kuchukua kwa ajili ya kujiandaa. Muhimu zaidi ni kuandaa itifaki yenu ya Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi. Sehemu hii pia inashauri kuhusu kuchukua hatua za kuelewa zaidi kuwahusu wawekezaji/ waandaaji wa mradi kwa ajili ya kujua ni akina nani hasa, na ni nani anayefadhili kazi yao. • Sehemu ya 3 inaeleza kile ambacho jamii za asili zinaweza kufanya wakati wa mchakato wa majadiliano kuhusu Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi, ikiwa ni pamoja na kupata usaidizi wa kisheria na kitaalamu, kuhakikisha kuwa una taarifa kamili, inayomtaka mwekezaji kupunguza hatari za mradi na kujadiliana faida mtakazopata kutokana na mradi baada ya kuridhia ardhi yenu ichukuliwe. • Sehemu ya 4 inaeleza aina mbalimbali za hatua za ufuatiliaji ambazo jamii ya watu wa asili inaweza kuchukua baada ya kukamilika kwa mchakato wa mashauriano kuhusu Haki ya Kujulishwa, Kuelewa na Kukubali kwa Hiyari kabla ya Kufanya Maamuzi. Inafafanua kile mnachohitaji kufanya kwa ajili ya kulinda haki zenu ikiwa mliukubali mradi, na kile mnachoweza kufanya ili kutetea uamuzi wenu wa kutoridhia mradi.